Tumia azam decoder kwa tv zaid ya moja

KING'AMUZI CHA AZAM TV KINAWEZA KUGAWA PICHA TV ZAIDI YA MOJA!?

Leo utapata jibu sahihi la swali hili:-

Jibu la swali hili linaweza likawa NDIO inawezekana king’amuzi cha Azam tv kugawa picha kwenye tv nyengine ( tv zaidi ya moja ).

NJIA ZA KUTUMIA

1.Kutumia HDMI na AV cable.


HDMI Cable

AV Cable

King’amuzi cha Azam ni HD hivyo kina uwezo wa kutumia cable ya AV na ya HDMI kwa wakati mmoja ila njia hii  inakulazimu kuwe na ukaribu kati ya kinapokaa king’amuzi na zinapokaa tv kwakuwa AV cable ikisafiri umbali mrefu hupoteza ubora wa picha na hata sauti,alkadharika kwa upande wa HDMI cable yenyewe ni nadra sana kupata zenye urefu wa zaidi ya mt 50 pia ni expensive kununua.Njia hii pia inauwezo wa kugawa tv kwa idadi uitakayo kwakuwa kuna kifaa cha kugawa ikiwa utatumia HDMI ama AV cable,ukitumia HDMI cable unatumia HDMI SPLITTER 

na ukitumia AV cable unatumia AV SPLITTER

.

2.Kutumia RF MODULATOR/RF CONVERTOR SWITCH


King’amuzi cha Azam tv hakina RF OUT ( RF OUT ni port inayotoa picha na sauti kwenye king’amuzi na kupeleka kwenye tv nyengine,kwenye tv inayoenda picha inaingia kwenye port inayoitwa RF IN/ANTENNA IN. )

.Kutumia Switch kutawezesha kubadili AV kuwa RF ( Unachomeka AV cable kwenye king’amuzi,kisha unachomeka kwenye SWITCH,alafu unafunga Coaxial cable ( Signal Cable ) kwenye port ya FR OUT ),Cable inayotoka kwenye Switch unaweza ukafunga SPLITTER

 itakayogawa kwa idadi ya tv uliyonayo.. Unaweza ukatumia Signal Amplifier ikiwa idadi ya tv ni nyingi ama umvali ni mrefu wa zilipo tv nyengine ili ubora wa picha uwe mzuri.

Zingatia: Njia namba 2 unaweza ukachanganya na ving’amuzi nyengine katika kugawa picha kwenye tv nyengine lakini namba 1 huwezi kufanya hivyo.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KULIPIA DSTV (Follow these simple steps to pay or top up your account)

SEA PIANO SUBWOOFER